
Mbunge wa Mumias East mheshimiwa Peter Kalerwa Salasya alifurushwa ugani Nyayo Jumapili muda mfupi tu baada ya kuketi tayari kushuhudia mechi baina ya Kenya Harambee Stars na Gaboni.
https://cliffmediatv.com/2025/03/23/peter-salasya-forced-out-of-nyayo-before-kenya-gabon-match/: Mheshimiwa Peter Salasya afurushwa ugani NyayoMuda mfupi tu baada ya Salasya kuket kwenye jukwaa, kundi la vijana walioonekana na gadhabu walimshambulia na kumtoa alikokuwa ameketi na kuanza kumharakisha huku wengine wakionekana kumrushia vitu.
Kwenye kanda ya video ambayo imesambaa mitandaoni inaonyesha mheshimiwa Salasya akiwa kwa hali ya kuvamiwa na kikundi cha vijana waliojawa gadhabu.
Kwenye kanda hiyo, vijana wanaskika wakimwamrisha mheshimiwa salasya kumheshimu Raila odinga na Raisi Ruto huku wakimweleza kuwa Raila Odinga sio rika yake. “Heshimu Raila odinga” vichana hao waliskika wakivoka kwa hasira.
Mheshimiwa Salasya aliokolewa na kuelekezwa nje ya lango la Nyayo kwa usalama wake na baadaye anaonekana akiwa ameketi bila shati lake huku akiwasuta vijana hao kwa madai kuwa walikuwa wanataka kumuua.